Ufunuo wa Yohana 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 7 (Swahili) Revelation 7 (English)

Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Ufunuo wa Yohana 7:1

After this, I saw four angels standing at the four corners of the earth, holding the four winds of the earth, so that no wind would blow on the earth, or on the sea, or on any tree.

Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, Ufunuo wa Yohana 7:2

I saw another angel ascend from the sunrise, having the seal of the living God. He cried with a loud voice to the four angels to whom it was given to harm the earth and the sea,

akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Ufunuo wa Yohana 7:3

saying, "Don't harm the earth, neither the sea, nor the trees, until we have sealed the bondservants of our God on their foreheads!"

Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu. Ufunuo wa Yohana 7:4

I heard the number of those who were sealed, one hundred forty-four thousand, sealed out of every tribe of the children of Israel:

Wa kabila ya Yuda kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Wa kabila ya Reubeni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Gadi kumi na mbili elfu. Ufunuo wa Yohana 7:5

Of the tribe of Judah were sealed twelve thousand, Of the tribe of Reuben twelve thousand, Of the tribe of Gad twelve thousand,

Wa kabila ya Asheri kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Naftali kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Manase kumi na mbili elfu. Ufunuo wa Yohana 7:6

Of the tribe of Asher twelve thousand, Of the tribe of Naphtali twelve thousand, Of the tribe of Manasseh twelve thousand,

Wa kabila ya Simeoni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Lawi kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Isakari kumi na mbili elfu. Ufunuo wa Yohana 7:7

Of the tribe of Simeon twelve thousand, Of the tribe of Levi twelve thousand, Of the tribe of Issachar twelve thousand,

Wa kabila ya Zabuloni kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Yusufu kumi na mbili elfu. Wa kabila ya Benyamini kumi na mbili elfu waliotiwa muhuri. Ufunuo wa Yohana 7:8

Of the tribe of Zebulun twelve thousand, Of the tribe of Joseph twelve thousand, Of the tribe of Benjamin were sealed twelve thousand.

Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-Kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; Ufunuo wa Yohana 7:9

After these things I looked, and behold, a great multitude, which no man could number, out of every nation and of all tribes, peoples, and languages, standing before the throne and before the Lamb, dressed in white robes, with palm branches in their hands.

wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 7:10

They cried with a loud voice, saying, "Salvation be to our God, who sits on the throne, and to the Lamb!"

Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, Ufunuo wa Yohana 7:11

All the angels were standing around the throne, the elders, and the four living creatures; and they fell on their faces before his throne, and worshiped God,

wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina. Ufunuo wa Yohana 7:12

saying, "Amen! Blessing, glory, wisdom, thanksgiving, honor, power, and might, be to our God forever and ever! Amen."

Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa waliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Na wametoka wapi? Ufunuo wa Yohana 7:13

One of the elders answered, saying to me, "These who are arrayed in white robes, who are they, and from where did they come?"

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo. Ufunuo wa Yohana 7:14

I told him, "My lord, you know." He said to me, "These are those who came out of the great tribulation. They washed their robes, and made them white in the Lamb's blood.

Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Ufunuo wa Yohana 7:15

Therefore they are before the throne of God, they serve him day and night in his temple. He who sits on the throne will spread his tent over them.

Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Ufunuo wa Yohana 7:16

They will never be hungry, neither thirsty any more; neither will the sun beat on them, nor any heat;

Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao. Ufunuo wa Yohana 7:17

for the Lamb who is in the midst of the throne shepherds them, and leads them to springs of waters of life. And God will wipe away every tear from their eyes."